Vijana wamtaja baba yao gaidi baada ya mauaji ya mama yao na mdogo wao

Luke na Ryan wamesimulia jinsi baba yao mzazi Lance Hart (57) alivyofanya tukio la kikatili kwa kumuuwa mama yao Claire (50) pamoja na mdogo wao wa kike Charlotte (19) na kisha na yeye kujiuwa kwa kujifyatulia risasi.

Luka na Ryna wakiwa na mdogo wao Charlotte enzi za uhai wake
Vijana hao wawili wameeleza kuwa katika maisha yao wamesumbuka sana kuvumilia vitendo vya baba yao vya kutaka kumdhibiti kila mtu. Mauaji hayo yalitokea siku chache baada mama yao kuamua kuondoka katika nyumba ya familia kutokana na mzozo uliokuwepo kati yao kwa kipindi hicho.

Picha ya marehemu Lance Hart ambaye amemuuwa mkewe na mtoto wake
Wakiongea katika kipindi cha Victoria Derbyshire, Luke (27) amesema, “”Hakuwa na jambo la maana la kumfanya aishi kuliko kutuuwa. Mtu kama baba yetu alikuwa gaidi, alikuwa anapanga kutuuwa wote watatu wiki tatu kabla ya kumuua mama na mdogo wetu aliyekuwa akisoma chuo.”

Claire pamoja Charlotte enzi za uhai wao
Naye Ryan (26) alisema, “Magazeti mengi yalikiandika juu ya baba yangu ni kwamba alikuwa mtu mwema na hata kutaka kutetea kile alichofanyika. Sio kuhusu maisha ya mama na Charlotte ila kumuhurumia yeye pale mateso ya hisia yanapoongelewa muathiriwa husahaulika. Hakuna aina nyingine ya mauaji ambapo muathiriwa hulaumiwa.”

Charlotte kabla ya kuuliwa akiwa na kaka yake Ryan.
Baada ya tukio hilo marehemu alikuwa ameacha ujumbe wenye kurasa 12 ambapo ya ujumbe uliokuwepo ndani yake ulisomeka, “Kisasi ni chakula baridi kinachogawiwa kwa walaji.” Hata hivyo baadhi ya ripoti zilinukuliwa kutoka kwa majirani zilimueleza Hart kama mwanaume mzuri sana ambaye alihakikisha ndoa yake haivunjiki.

Comments