Uongozi wa Simba SC wanyoosha maelezo kuhusu tetesi za kuporwa kwa wachezaji wake na Singida United

Baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa Singida United imekwapua wachezaji watatu kutoka Simba SC, leo Makamu wa Rais wa klabu ya hiyo, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amekanusha taarifa za kuondoka kwa wachezaji hao watatu ambao ni Ibrahim Ajib Migomba, Jonas Gerard Mkude na Abdi Hassan Banda katika kipindi hiki cha usajili.
Tokeo la picha la kaburu nyange
Makamu wa Rais wa klabu ya Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’
Kaburu amesema kwa sasa Klabu hiyo haina mpango wa kuuza mchezaji yoyote kwani Simba SC msimu ujao itakuwa na mashindano ya kimataifa .
Taarifa za kutaka kuondoka, sisi kama viongozi tunazisikia na kuziona katika vyombo vya habari, lakini ninakuhakikishia hakuna hata mmoja atakaeondoka katika kipindi hiki,kwani klabu yetu ipo kwenye mashindano ya kimataifa kwa msimu” amesema Kaburu.
Katika kukazia hilo Kaburu amesema tayari wachezaji hao watatu wameshaanza mazungumzo ya kusaini mikataba mpya ambayo itawawezesha kuendelea kuitumikia klabu ya Simba kwa kipindi kingine, na amesisitiza kuwa katika hatua nzuri ya kukamilisha mpango huo.
“Wachezaji wetu wote watatu wapo katika hatua nzuri ya kusaini mikataba mipya, tunataka kuona Simba inaendelea kuwa imara kwa kuwatumia watu hawa ambao msimu huu wameonyesha kuwa muhimili mkubwa katika klabu yetu.”amesema ‘Kaburu’ kwenye mahojiano yake na Times FM.
Hata hivyo amekiri wazi kuwa kuna ofa ya moja ya klabu kubwa ya ligi kuu ya soka Tanzania bara, lakini hakua tayari kuitaja klabu hiyo na hawafikirii kumuuza ni heri akacheze nje ya nchi

Comments