Tutegemee album ya Ngwear – M2 the P

Ikiwa ni miaka minne tangu rapa, Albert Mangwear maarufu kama Ngwea afariki dunia nchini Afrika Kusini tarehe 28/5, aliyekuwa swahiba wake M2 the P ameeleza mikakati ya ujio wa album ya msanii huyo.

Akiongea na Byno na Joco wa Sibuka Fm kupitia kipindi cha 180 Power, M2 theP amesema ifikapo mwezi june mwaka huu wanatarajia kutoa album ya Ngwear yenye nyimbo sita za marehemu Ngwear.

M2the P
“Ifikapo mwezi wa sita ama mwisho wa mwezi  huo nadhani album ya Cow Obama yenye nyimbo sita inatakuja ,watu wakae tayari ndani ya Foundation ya Cow Obama (Ngwear) ambayo ndani yake wapo watu kama P-Funk Majani, Brother Dr Kenny na M2theP” amesema M2 the P.
Pia msanii huyo amesisitiza  kuwa watu wauendelea kusikiliza mziki mzuri tokea kwake, na kwa mwaka huu wameshindwa kufanya tamasha la kumuenzi Ngwear kutokana na kuingiliana kwa mwezi mtukufu wa ramadahani.
 

Comments