Tox Star akaribia kumburuza mahakamani Belle 9

Tox Star baada ya kuahidi kuachia wimbo wa ‘Masumu ya Mapenzi’ kwa kukopi jina la wimbo wa Belle 9 aliuachia miaka iliyopita kutokana na kitendo cha kuiba wimbo wake sasa msanii huyo amebadili mawazo na kuamua kukwenda mahakamani.

Hit maker wa Pretty Girl ambao alimshirikisha Alikiba na kufanya vizuri kipindi hicho, amesema anafikiria kwenda mahakamani kuwashitaki Belle9 na G Nako kwa kutumia Idea ya ngoma yake ya ‘Ole’ aliouachia mwaka 2014.
“Watu wamenikana lakini naamini wao watanitafuta kwa sababu kila kitu kina sheria ujue” amesema muimbaji huyo wakati akiongea katika kipindi cha Zero Planet cha Ice FM.
“Nilikua namsubiri wakili wangu, wakili wangu anaingia leo akiingia leo na sisi baadae tutaongea naye na tutajua nini cha kufanya. Wao si wamenikana bwana basi ngoja mimi niende mbele zaidi. Ushahidi ninao mimi nilimeachia 2014 wao wameachia mwaka huu kwahiyo ushahidi unaonesha mimi ndio nilianza kabla yao,” ameongeza
Alipoulizwa kuhusu Haki Miliki ya wimbo huo ambao ni kitu kimekuwa kikiwatesa wasanii wengi wa Bongo Flava, Tox amesema huenda hiko kitu ndio kikaanzia kwake.

Comments