Sina mchumba kwa sababu… – Snura

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Snura amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hana mume wala mchumba mara baada ya kuzinguana na mpenzi wake ambaye walizaa nae mtoto mmoja wa pili.
Snura
Akizungumza na kipindi cha Kwetu Fleva cha Magic Fm Snura amesema sababu ya kuachana na mpenzi wake ni baada ya yeye kumkimbia alipokuwa mjamzito na hata alipojifungua hakutaka kumuhudumia mtoto.
“Mimi bado sijaolewa wala siishi na mtu (mpenzi) naishi na mama yangu na watoto wangu, sina mchumba kwa sababu mchumba ni yule ambaye amekuja kujitambulisha kwa wazazi wangu.Tulishindwana na baba watoto wangu kwa sababu hataki kulea mtoto.
“Mwanzoni mapenzi yalikuwa motomoto hadi nikapata ujauzito, ikatoka na barua ya uchumba lakini mimba ilipofika mwezi mmoja akahisi kama kuna majukumu hapa akaanza kubadilika lakini mimi sikujali nikalea mimba hadi ikafikisha miezi tisa nikajifungua,” amesema Snura.
Snura amesema mara baada ya kujifungua alimjulisha mpenzi wake huyo lakini hakupata msaada wowote na kilichomuumiza zaidi si kwamba hakuwa na uwezo kwani ni mtu ambaye alikuwa anajimudu kiuchumi.
“Hata mtoto aumwe hakutumii hata sh. 10, nikawa nimeficha nikaja kuongea mtoto ana mwaka na zaidi kwa sababu nimeona huu ni ujinga.  Ubaba wa picha, akipost picha instagram ndio mtoto ameshakula na ameshasoma, ikabidi nimwambie mwenzangu ubaba huo wa picha nimeshindwa,” ameeleza Snura.

Comments