Reli ya kisasa ‘standard gauge’ yazinduliwa rasmi nchini Kenya (+Picha)

Leo ni siku nzuri sana kwa wakenya wanaoishi au wenye ndugu zao kwenye miji ya Mombasa na Nairobi kwani adha ya usafiri wa ardhini haitakuwepo tena baada ya uzinduzi wa reli ya kisasa ya kiwango cha kati (Standard Gauge) ambayo itawapungunguzia adha zote za usafiri ikiwemo muda.
Rais Kenyata kwenye uzinduzi wa reli ya kisasa mapema leo mjini Mombasa.
Uzinduzi huo wa reli ya kisasa uliofanyika leo mapema mjini Mombasa na rais wa Kenya, Uhuru Kenyata umeigharimu Kenya kiasi cha bilioni 327 za Kenya na unatarajiwa kuchochea sekta ya uchukuzi na usafirishaji kati ya miji hiyo mikubwa ya kibiashara nchini Kenya.


Treni za mizigo zilianza kazi jana na ile ya abiria iliyopewa jina la Madaraka Express imeanza kazi leo kwa kusafirisha abiria kutoka Mombasa hadi Nairobi.

Treni hizo zinazotembea umbali wa kilometa 120 kwa saa zitatumia masaa manne tuu kusafirisha abiria au mizigo kati ya Mombasa na Nairobi.

Kuhusu nauli ya Treni hizo kwa daraja la kawaida tiketi zitauzwa kwa Ksh 900 huku daraja la biashara nauli ikiwa ni Ksh 3000.Tazama picha za uzinduzi wa Reli hiyo ya kisasa na nyingine zinazoonesha kila kituo kutoka Mombasa hadi nairobi.



Muonekano wa ndani wa mabehewa ya daraja la kawaida
Ndani ya behewa la VIP




















Picha ikiwa imepigwa kwa ndani ya Treni muonekano wa nje ukiwa safarini

 

Comments