Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutoyapiga faini makampuni ya simu atakayoshindwa kujiunga na Soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) badala yake wayafute.
Rais Magufuli amesema hayo leo Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakati akizindua mfumo mpya wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki.
“Tulitangaza makampuni ya simu yajiunge na DSE na yamejizungusha na ni Vodacom pekee walijiunga. Makampuni ya simu kama mnajiamini kuwa mnalipa kodi, mnaogopa nini kujiunga na DSE tuone mapato yenu? TCRA, makampuni ya simu ambayo hayajajiorodhesha DSE msiyapige faini, yafuteni. Ni lazima tutoe maamuzi hata kama yanauma,” alisisitiza Rais Magufuli.
Hata hivyo Rais Magufuli ameyataka makampuni ya simu na mabenki kujisajili kwenye mfumo huo ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi za serikali kwa uharaka na uaminifu zaidi.

Comments
Post a Comment