Nilijua ndoa yangu na Kris Humphries haitadumu-Kim

Baada ya ndoa ya Kanye West na Kim Kardashian kutimiza miaka mitatu, Kim  amefunguka kuizungumzia ndoa yake ya zamani na mcheza kikapu, Kris Humphries iliyodumu kwa saa 72 tu.

Kupitia kipindi cha Watch What Happens Live na mtangazaji, Andy Cohe, Kim amedai kuwa siku ya fungate aligundua ndoa yake hiyo aliyofunga kwa siri na mchezaji huyo wa basketball  haitadumu muda mrefu.

Enzi za ndoa ya Kim Kardashian na Kris Humphries mwaka 2010
“Nilitaka kuolewa kipindi hicho ndio maana nikaolewa na Humphries, na wasichana wengi wanaolewa kutokana na kuwaona kuona marafiki zao wana watoto na wao hujikuta wanaitamani ile hali, ndicho kinachotokea na kilichonitokea mimi” amesema Kim.
Ndoa ya Kim na Humprey ilifungwa kwa siri ikihusisha famila zao tu bila hata marafiki na ilifungwa maeneo ya Montecito, California, estate .
Hata hivyo ndoa hiyo haikudumu baada ya Kim Kardashian  kuachana na mwanaume huyo na kupewa taraka yake.

Comments