Msanii wa Hip Hop nchini Tanzania, Nikki Mbishi amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kumtaka atupie jicho juu ya uendeshaji wa mradi wa mabasi ya mwendokasi (DART) hususani suala la kujaza watu ‘Seat Level’ ili mradi huo uweze kudumu kwa muda mrefu.
Nikki Mbishi amesema kwa sasa haoni umuhimu wa Mabasi hayo kwani watu wanajazana kama daladala huku akidai endapo hali hiyo itaendelea basi mradi huo uliogharimu mamilioni ya pesa utakufa hata kabla ya miaka mitatu .
“Bora daladala za kawaida tu,#Mwendokasi wameishia kuzindua ila hawafuatilii utendaji…After 3years yote yameoza, #MWENDOKASI watu wanajazana kama 3rd class train ya INDIA yatadumu kweli?.“ameandika Nikki Mbishi kwenye ukurasa wake wa Twitter huku akimshauri Rais Magufuli kuingilia kati tatizo hilo ili kunusuru mradi huo unaoonekana kuelemewa na wateja
“Hadhi ya#Mwendokasi ni level seat sio kushonana kama #Embe toka Kibada. Mzee @MagufuliJP tazama hilo. Mradi unakufa soon“,ameandika Nikki Mbishi.
Kwasasa magari ya mwendokasi kwenye vituo vikubwa yamekuwa yakilemewa na wateja kiasi kwamba wateja huzalizika kugombaniana magari hayo kama ilivyokuwa kwenye daladala za kawaida.
Nikki Mbishi amesema kwa sasa haoni umuhimu wa Mabasi hayo kwani watu wanajazana kama daladala huku akidai endapo hali hiyo itaendelea basi mradi huo uliogharimu mamilioni ya pesa utakufa hata kabla ya miaka mitatu .
“Bora daladala za kawaida tu,
“Hadhi ya
Kwasasa magari ya mwendokasi kwenye vituo vikubwa yamekuwa yakilemewa na wateja kiasi kwamba wateja huzalizika kugombaniana magari hayo kama ilivyokuwa kwenye daladala za kawaida.
Comments
Post a Comment