Producer mkubwa wa muziki Marekani Jermaine Dupri amelalamikia tabia ya vijana wa kizazi kipya kuanza kufanya hiphop na rap bila kujifunza historia ya muziki huo ‘History Of Hip Hop Culture’.
Dupri ambaye kwa sasa anatengeneza kipindi cha tv cha vijana wadogo wanaotaka kuwa wasanii wakubwa wa hiphop amesema ni aibu kusikia msanii mkubwa anasema hajawahi kumsikiliza Notorious B.I.G.Dupri anasema “Anagalia Lil Yachty anasema hajawahi kusikiliza muziki wa Biggie, watu walishanga nakusema Mungu wangu, hiki ni nini sasa ?, ila mimi niliona ni mtoto tu ambaye hajawahi kusikiliza muziki a B.I.G,ni muhimu wajifunze historia”
Lil Yachty alikuja baadae kulalamika kuwa kauli hio ilitafsiriwa vibaya, nakusema yeye hakuata nafasi ya kuzikiliza wasanii wengi kutoka New York.
Comments
Post a Comment