Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Navio amechaguliwa kuwa mmoja ya wageni maalum watakaohudhuria katika uzinduzi wa tuzo za Africa HipHop Award mjini Lusaka, Zambia Julai 1 ya mwaka huu.
Navio ametoa taarifa hizo kupitia mtandao wa Instagram, ambapo ameweka cover inayoonyesha tarehe ya uzinduzi wa tuzo hizo ambazo zitafanyika katika ukumbi wa Chez Ntemba.
Pia kupitia tovuti ya waandaaji wa tuzo hizo, wameweka baadhi ya picha za wasanii wa Afrika ambao wanafanya muziki wa Hip Hop. Baadhi ya picha za wasanii zilizowekwa katika tovuti hiyo ni ile Fid Q, AKA, Cassper Nyovest na wengine.

Comments
Post a Comment