Msanii mpya ndani ya Lebo ya WCB, Lava Lava amesema haofii kufunikwa siku akitoa wimbo na masanii yeyote kutoka ndani ya lebo hiyo kwani kila mmoja ana mashabiki wake.
Akizungumza kwenye kipindi cha Papaso cha TBC Fm, Lava Lava amesema WCB ni familia ambayo inafanya kazi kwa ushirikiano na kuelekezana hivyo suala la kufunikana halipo.
“Wasanii wa WCB wote ni wazuri na wakali kabisa, tena ukikaa unasema hii sehemu nitapitaje hapa lakini mwisho wa siku kitu ambacho kinanipa moyo ni kwamba hadi umeona uongozi umekaa na kuamua kunitoa mimi kunipeleka mbele za watu ujue kuna kitu kwangu. Msanii yeyote waWCB nipo tayari kufanya nae kazi… kufunikwa ipo ila mwisho wa siku kila mtu ana mashabiki wake,” amesema Lava Lava.
Lava Lava ni msanii wa tano kujiunga na WCB mara baada ya Harmonize, Rayvanny, Queen Darleen na Rich Mavoko. Wimbo wake wa kwanza kutoa unaitwa ‘Tuachane’ ambao unafanya vizuri kwa sasa.

Comments
Post a Comment