Msanii wa Bongo Fleva, Barnaba amewataka wasanii wenzake kutopenda kuongea sana katika vyombo vya habari kama hamna ulazima wa kufanya hivyo hasa pale wanapoyumba kimuziki.
Barnaba amesema kuna wasanii kila mara ni kusema kuweni tayari kwa ujio wangu hadi inafika wakati unajiuliza tuwe tayari mara ngapi? na kuongeza kuwa muda mwingine kutokuongea kuna kunaongeza thamani kama msanii atajielewa.
“Kuna wengine wanaamini wakiongea sana ndio wanapata respect official ya kusikika sana, na kuna wengine wakifanya hivyo wanafanikiwa kutokana na vitu wanavyovibuni. Lakini saa nyingine kama huna cha kuongea na sio muhimu sana kuongea kwa muda huo kwa nini usikae kimya,” Barnaba ameimbia Times Fm.
Barnaba amesema wasanii inabidi watofautishe kuyumba kimuziki na kuyumba maisha ya kimuziki,Kuyumba kimuziki ni ile msanii anatoka track ya kwanza mbovu, ya pili mbovu, au ametoa haijapokelewa vizuri kama nyimbo za awali.
“Na kuna kuyumba kimaisha ya kimuziki, wasanii tunaishi katika maishi ya kimuziki ambayo muda mwingine ni mabaya sana ambayo ukiyumba hapa unayumba hadi kimuziki. Lazima ujikwae ili uitafute namba moja, kwa hiyo kujikwa ni siri ya mafanikio katika maisha au siri ya kuyumba katika maisha ya kimuziki, kwa mtu mwenye akili maana yake unajifunza zaidi,”amesema Barnaba.

Comments
Post a Comment