Harmorapa ni ‘kichaa wa kiki’ – Gigy Money

Video Vixen, Gigy Money amefunguka na kusema msanii wa Bongo Fleva, Harmorapa anapenda kiki hadi anapitiliza, kitendo kinachopelekea kumuita kichaa wa kiki, na watu wanavyomfananisha na Harmonize sio sawa kwani hawafanani hata kidogo.
Gigy Money na Harmorapa
Gigy Money ameiambia Hotmixmziray kuwa, Harmorapa anapenda kiki ambazo haziendani na umri wake na ilifika wakati akamtafuta ili wapige picha kwa ajili ya kutengeneza kiki ila yeye na meneja wake hawakuwa na fedha za kumlipa.
“Unaponipa nafasi ya kumzungumzia Harmorapa tayari ni kiki kwake, ila ni kichwaa, kwa kiki!, nampenda yule ni chizi kiki. Unajua siku ile alikuwa kweli anaogopa ile bastola lakini kwa kuwa alifuata kiki alikubali tu akimbie adhaalilike.
Gigy Money
“Yule aliniita anataka kiki, hela hawana na meneja wake, watoto wadogo ndio wanavurungwa nae wanapiga picha naye, alikutana na mimi akapiga picha akaipost mara sita. Kusema anafana na Harmonize wanakosea sana, Harmonize is very handsome halafu ana baby mzungu lakini Harmorapa atamtoa wapi baby mzungu, ataishia kushoot nao video tu,” amesema Gigy Money.
Harmorapa
Katika hatua nyingine Gigy Money amesema anatarajia kutoa wimbo uitwao Shobo ambao amepanga kumshirikisha Nay wa Mitego licha ya kuwa bado hawajakaa na kuongea.
“Wimbo unahusisha watu wote waliojaribu ‘kukwichi’ na Gigy, yaani Tekno, Alibiba, Abukiba, Rich Mavoko yaani wote ambao unajua walishasikika na Gigy huku ndani wamepita.  Mwanasheria itabidi niongeze kipande chake, ni wimbo wa maisha yangu,” amesema Gigy Money.

Comments