Familia ya mwanamuziki Chris Cornell aliyefariki Mei 18 na kuzikwa wiki iliopita maeneo ya Hollywood Forever Cemetery, imekataa kuzungumzia sababu ya kifo cha ndugu yao huyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, familia hiyo imesema kuwa bado uchunguzi kuhusu kifo cha Cornell unaendelea. Mwanasheria wa familia hiyo Kirk Pasich amesema kuwa kuachiwa kwa uhuru wa kuongelea suala hilo kunaweza kuingilia na kuharibu uchunguzi unaofanywa na polisi.
“Tunashangazwa na taarifa iliyotolewa na kituo cha afya kilichofanyia uchunguzi wa mwili wa marehemu kusema kuwa tukio hilo ni lakukusudiwa [Marehemu aliamua kujiua],” imesema familia hiyo.
Wakati huo huo mke wa marehemu Vicky, ameeleza kuwa familia hiyo imekuwa na maswali mengi kuhusu tukio hilo na ripoti iliyotolewa hivyo wanasubira taarifa ya toxicology itakayoondoa utata uliopo sasa

Comments
Post a Comment