Chelsea yalipwa Paundi milioni 150.8

Chelsea ni mabingwa wa ligi ya England 2016-17
Chelsea ni mabingwa wa ligi ya England 2016-17
Klabu ya soka ya Chelsea imelipwa paundi milioni 150.8 na chama cha soka cha England FA baada ya kushinda ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2016-17.
Msimu wa 2015-16 ulishuhudia ongezeko kubwa kwa mkataba wa matangazo ya Televisheni ukitoa takriban Paundi bilioni 2.4 kwa timu 20 zaidi ya msimu uliopita zilipolipwa Paundi bilioni 1.6.
Timu iliyoshika mkia kabisa Sunderland imepata Paundi milioni 93.471.
Fedha hizo zinatokana na matangazo ya Televisheni, mikataba ya kibiashara sambamba na zawadi

Comments