Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Zuberi Kabwe, ametoa shukrani kwa Bunge la Tanzania kwa kumsamehe Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa kuendelea na vikao vya Bunge.
Mbunge Zitto ametumia ukurasa wake wa Facebook kutoa shukrani hizo kwa bunge. Ameandika hivi:
Mbunge Zitto ametumia ukurasa wake wa Facebook kutoa shukrani hizo kwa bunge. Ameandika hivi:
Hatimaye Waziri Kivuli wa Fedha ndg. Halima Mdee amesamehewa na ataendelea na vikao vya Bunge. Hii ndio haki. Mtu aliomba radhi hadharani, kwanini aadhibiwe. Shukran Kwa Bunge.Halima Mdee alituhumiwa kutumia lugha chafu bungeni wakati wa uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki, Aprili 14 mwaka huu
Comments
Post a Comment