Wanajeshi waliogoma waliteka mji wa Bouaké ambao ni pili kwa ukubwa nchini humo
Mkuu wa majeshi wa Ivory Coast ametangaza katika kituo cha televisheni kuwa serikali imefikia makubaliano na wanajeshi waliogoma na kuhaidi kulipa madai yao ndani ya siku nne.
Lakini wazungumzaji wawili wa wanajeshi hao wamesema wamekataa ombi hilo na kuitaka serikali imlipe kila mwanajeshi francs milioni tano mpaka saba karibia dola 12,000.Karibia wanajeshi elfu nane wamejiingiza kuipinga serikli, baada ya kushindwa kulipwa nyongeza ya fedha walizohaidiwa.
Comments
Post a Comment