Wanajeshi kukabiliana na maandamano Venezuela

Polisi wametumia mabomu ya machozi lakini bado hawajaweza kudhibiti maandamano hayo
Polisi wametumia mabomu ya machozi lakini bado hawajaweza kudhibiti maandamano hayo
Serikali ya Venezuela imesema ni muhimu kuwepo kwa vikosi vyake vya jeshi katika mji wa Tachira ulio karibu na mpaka wa Colombia.
Waziri wa ulinzi amesema zaidi ya wanajeshi elfu mbili watatumwa eneo hilo kukabiliana na maandamano yanayoendelea dhidi ya serikali.
Mapema wiki hii kijana wa miaka 15 aliuawa katika mji huo alipokuwa akinunua maua kwa ajili ya mama yake.
Waandamanaji wamekuwa wakivaa vifaa maalum kuzuiwa kuathiriwa na gezi ya machozi
Waandamanaji wamekuwa wakivaa vifaa maalum kuzuiwa kuathiriwa na gezi ya machozi
Kwa wiki hii pekee wameuawa watu watatu katika eneo hilo kutokana na maandamano yanayoendelea.
Kwa nchi nzima mpaka sasa wameuawa zaidi ya watu 43 kwa maandamano yaliyodumu chini ya miezi miwili.
Raia sita wa Colombia walikamatwa mjini Tachira kwa kudaiwa kuchochea maandamano hayo.

Comments