Jamii kutoka Arnhem mashariki wakicheza dansi ya kitamaduni katika ufunguzi wa kikao Uluru
Viongiozi wa kijadi nchini Australia ambao wamekua wakikutana kujadili jinsi ya kutambuliwa na katiba ya nchi watatangaza azimio la pamoja Ijumaa.
Viongozi 250 wanakutana katika eneo la Uluru, ambapo ni chimbuko asili ya jamii za Aborigine tangu jadi. Katiba ya Australia haitambui jamii asilia wala kuweka mikakati ya kuwalinda dhidi ya ubaguzi.
Kongamano la sasa linanuia kuwepo na azimio la pamoja kuhusu jamii asili za nchi hiyo.
Aidha azimio la Uluru linanuiwa kuwasilishwa kwa kura ya maoni ya kitaifa.
Jamii hii inaomba siyo tu kutambuliwa kisheria, lakini kuwa na uwakilishi maalum bungeni na nyathifa nyingine muhimu za kitaifa.
Pia wanataka kulipwa fidia kutokana na dhuluma za kihistoria.
Comments
Post a Comment