Rais Trump, tayari amewasili Sicily
Viongozi wa mataifa saba yenye nguvu za kiuchumi duniani maarufu kama G saba, leo wanaanza mkutano wao wa siku mbili nchini Italia.
Mkutano huo unaofanyika Sicily utakuwa wa kwanza wa mataifa saba yenye nguvu, kuhudhuriwa na Rais Trump katika siku za mwisho ya ziara yake nje ya nchi yake.Mkutano huo unafanyika pia katika wiki hii ambayo mashambulio ya kigaidi yalifanyika nchini Uingereza, huku viongozi hao wakitarajiwa kukubaliana juu ya haja ya kuongeza mapambano kukabili imani kali.
Comments
Post a Comment