Ukuta wawaua wageni 22 harusini India

Ukuta ulioanguka na kuwaua wageni 22 harusini India
Ukuta ulioanguka na kuwaua wageni 22 harusini India
               
Takriban watu 22 wamefariki baada ya ukuta kuwaangukia wakati wa harusi kaskazini mwa India.
Wageni hao walikuwa wamejikinga na mvua kubwa inayoendelea kunyesha kabla ya ukuta huo kuwaangukia.
Watu wengine 26 walijeruhiwa katika jali hiyo ya Bharatpur ,wilaya moja ya jimbo la Rajasthan ,15 kati yao wakiwa na majeraha mabaya.
Vyombo vya habari vinasema kuwa vibanda vya kuuza chakula vilikuwa vimewekwa kandakando ya ukuta huo karibu na harusi.
 
Ukuta huo na kibanda ulianguka kutokana na kimbunga kulingana na afisa wa Polisi Anil Tank aliyenukuliwa akisema.
Alisema kwamba ukuta huo wenye urefu wa futi 90 uliwaangukia wageni wengi.
''Waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali za eneo hilo mara moja huku wakipewa matibabu''.

Comments