Meneja wasanii kutoka WCB Babu Tale ameonesha hisia zake kuhusu ajira za Tanzania ambapo amedai kuwa tatizo la ajira limekuwa sugu huku likigusa pia familia yake baada ya mke wake kukosa kazi hadi sasa.
Babu Tale amedai pia kuwa licha ya mkewe kuwa na Degree anajutia fedha zake alizozipoteza kumsomeshea kwenye Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM.
“Msomi wangu bado yupo nyumbani na degree yake ipo kabatini nakumbuka nilisema ajira kamlete ila kwake imekua ngumu pamoja na connection zote nilizo nazo bado mtiani na hivi serikali imetangaza juu ya miaka 30 ajira hakuna pesa yangu imeenda bure IFM” – Babu Tale.
Comments
Post a Comment