‘Ukimya wangu haujasababishwa na kuoa’ – Amini

Msanii wa muziki, Amini amesema kukaa kimya kwenye muziki hakuja sababishwa na yeye kuoa bali amekuwa akijiandaa ili anaporudi ahakikishe anakuwepo muda wote na sio kwa kipindi kifupi.
Amini
Amini ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa kwa sasa amesharekodi nyimbo 10 kwa ajili ya ujio wake mpya.
“Kuwa kimya sio sababu ya kuoa kwangu, mimi huwa napenda kutoa vitu vizuri ili ninavyovitoa visiwe vinakwama, sio umetoa wimbo mmoja umetulia.  Kwa hiyo sasa hivi nimekaa kuandaa nyimbo ili ninapotoa nyimbo inakuwa ni nonstop. Kuna ngoma ambazo zipo tayari kwa kutoka, nimeandaa kama ngoma 10 na kuna nyimbo nyingine nimeziandika sijazirekodi.  Kwa hiyo nina nyimbo nyingi sana nilikuwa naanda kwa ajili ya kwenda kutikisa ulimwengu,” amesema Amini.

Comments