Trump: Nataka kuanza kuendesha nchi kwa umakini

Tuhuma ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani imegonga vichwa vya habari duniani kwa muda sasa
Tuhuma ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani imegonga vichwa vya habari duniani kwa muda sasa
Rais wa Marekani Donald Trump amesema anataka kuanza kuendesha nchi baada ya utawala wake kugubikwa na utata wa tuhuma za timu yake ya kampeni kushirikiana na Urusi.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Washington, akiwa pamoja na Rais wa Colombia ambae yuko ziarani nchini Marekani, amesema anaheshimu uteuzi wa mchunguzi maalumu, lakini akarudia kusema kuwa sakata hilo linaigawa nchi:
Rais Trump pia amekana kujaribu kuishawishi FBI katika uchunguzi wake kwa kumfuta kazi mkurugenzi wake James Comey.
Amemwelezea Comey kuwa hakuwa chaguo la watu.
 

Comments