
mwisho ya ziara ya kiongozi huyo mashariki ya kati.
Raia katika maeneo ya Gaza na ukingo uliokaliwa wa magharibi kupinga ziara hiyo na kuunga mkono wafungwa wa Palestina walioko katika magereza ya Israel waliogoma kula.
Jumatatu Trump alisema amekuja "kuhakikisha uhusiano usiovunjika" kati ya Marekani na Israel na kuna "nafasi iliyo adimu ya kuidhinisha usalama utulivu na amani kwa eneo hilo".
Aliwasili Tel Aviv kutoka Saudi Arabia ambako katika mkutano Jumapili aliwaomba viongozi wa kiislamu na kiarabu kuwatokomeza waislamu wenye itikadi kali.

Ameongeza kuwa "anashukuru" kwamba Abbas alihudhuria mkutano huko Riyadh na "kuahidi kuchukua hatua madhubuti zinazo hitajika kukabiliana na ugaidi na fikra zake za chuki".
"Amani haiwezi kuweko katika eneo ambapo ghasia zinaendekezwa, kufadhiliwa na pia kutuzwa," aliongeza, inavyoonekana ni kama anataja malipo yaliotolewa na utawala wa Palestina kwa familia za wafungwa wa Palestina na waliouawa katika mzozo na Israel.

Baadaye Jumanne Trump alirudi Jerusalem. alilitembelea eneo la kumbu kumbu la mauaji ya kimbari la Yad Vashem.
Comments
Post a Comment