
Trump atarajia mkutano wenye mafanikio
Rais wa Marekani Donald Trump anakutana na kiongozi wa utawala wa palestina Mahmoud Abbas wakati wa siku ya pili ya ziara yake Mashariki ya Kati
Waisrael na wapalestina hawajafanya mazungumzo ya moja kwa moja kwa zaidi ya miaka mitatu.Siku ya Jumatatu Trump alisema kuwa kuna ushirikiano mkubwa kati ya Marekani na Israel
Pia alionya juu ya kuwepo kwa tisho la Iran kwa amani ya dunia

Ziara huiyo ya siku mbili nchini Israel na katika utawala wa Palestina ni sehemu ya ziara ya ya kwanza ya kigeni ya bwana Trump.
Suala kuu ni kubuniwa kwa taifa huru la palestina kando ya Israel.

Baadhi ya watu wenye ushawishi ndani ya serikali ya Israel wanaamini kuwa ardhi hiyo ni ya Waisraeli waliyopewa na Mungu.
Comments
Post a Comment