Toni Braxton afunguka kwa mara ya kwanza kuhusu mahusiano yake na Birdman


R&B star Toni Braxton amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu mahusiano yake na boss wa Cash Money Bryan “Birdman” Williams.
Toni amedhibitisha kuwa mahusiano yake na Birdman ni yakimapenzi ila hataki kuwa na furaha sana sababu ni mapema na hajui kijacho kati yao.
Toni anasema sababu ya kuwa muoga wa kuingia kwenye mahusiano ni kutokana na kuwa SINGLE kwa muda mrefu.
Toni na Birdman walionekana pamoja kwenye tuzo za BET mwaka jana na kuzua gumzo kuhusu mahusiano yao.
Toni amekuwa single toka kutengana na mume wake Keri Lewis mwaka 2009, talaka ilikamilika mwaka 2013, wanawatoto wawili Denim na Diezel.

Comments