Timu hii yaongoza kuwa na vikombe vingi vya ubingwa Uingereza

Je unafahamu timu ya Uingereza ambayo inaongoza kubeba makombe mengi ya ubingwa? Basi chukua hii ni Manchester United.

Baada ya hapo jana usiku United kufanikiwa kubeba kombe la Europa League baada ya kuifunga Ajax kwa mabao 2-0 katika mchezo wa fainali, imefanikiwa kuweka rekodi ya kuwa na makombe 42 katika kabati lao.
Miongoni mwa makombe hayo ambayo imewahi kuchukua timu hiyo ni pamoja na ligi kuu mara 20, FA mara 12, kombe la ligi mara tano, kombe la Uefa mara tatu, na makombe mingine ya Ulaya 2.

Timu nyingine zinazofuatia ni pamoja na Liverpool ambayo wamefanikiwa kuweka vikombe 41 katika kabati lao na Arsenal vikombe 29.
Wengine ni Chelsea wana vikombe 22 vya ubingwa na Aston Villa viukombe 20.

Comments