The Fate of the Furious yatinga orodha ya filamu zilizoingiza fedha nyingi

Filamu ya Kampuni ya Universal Pictures ya The Fate of the Furious imetajwa kufikisha kiasi cha dola bilioni moja mpaka kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita.

Awali filamu hiyo ambayo iliingia sokoni mwezi April mwaka huu ilivunja rekodi kwa kuwa na ufunguzi mkubwa zaidi wa muda wote baada ya kuingiza dola milioni 532 kwenye majumba ya sinema duniani kote mwishoni mwa wiki yake ya kwanza tangu itoke.
Mpaka sasa filamu hiyo imetengeneza kiasi cha dola bilioni 1.223 na kuifanya kuwa filamu ya 11 kutengeneza fedha nyingi zaidi kwa muda wote hivyo kuifanya kuwa filamu ya 11 iliyoingiza fedha nyingi zaidi duniani katika muda wote.
Filamu hiyo imechezwa na mastaa kibao akiwemo Vin Diesel, Dwayne Johnson, Charlize Theron, Jason Statham, Michelle Rodriguez, Kurt Russell, Dame Helen Mirren, Scott Eastwood huku Felix Gray Gray akiwa ndio muongozaji wake.

Comments