TFF YAZIDI KUIUMIZA SIMBA

Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF), limesema linaendelea na uchunguzi kuhusiana na lile tukio la kishirikina lililofanywa na anaesadikika kuwa ni mwanachama wa Klabu ya Simba kwenye mchezo dhidi ya Azam FC.
Picha ikimuonesha shabiki wa Klabu ya Simba aliyehusisha na vitendo vya kishirikina.
Shabiki huyo aliyetambulika kwa majina ya Ngade Ngalambe, aliingia na kumwaga kimiminika ambacho baadae kilielezwa kuwa ni mafuta ya nguruwe.
Kitendo hicho kilitokea muda mchache kabla Simba haijavaana na Azam FC katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo Simba ilishinda kwa bao 1-0.
Tunaendelea kulifanyia uchunguzi suala hilo na endapo itabainika basi kanuni zipo wazi, hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya Simba na aliyefanya kitendo hicho,” Alisema Ofisa Habari wa TFF,Alfred Lucas mbele ya waandishi wa habari.
Hata hivyo bado TFF haijaweka wazi ni hatua gani za kisheria zitachukuliwa kwa klabu ya Simba endapo shabiki huyo atakutwa na hatia.

Comments