Singida United yamnasa Ibrahim Ajib

Baada ya kupata udhamini wa mamilioni kutoka kwa Kampuni ya kubashiri ya SportPesa sasa Klabu ya Singida United ni mwendo wa kusajili tu wachezaji wa kimataifa.
Image result for ibrahim ajibu
Ibrahim Ajib
Kwani baada ya kuwapora wachezaji tegemezi wa Klabu ya Tusker na Caps United ya Zimbabwe, awamu hii wamewatikisa mabingwa wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara, Simba SC kwa kumalizana na mshambuliaji wao Ibrahim Ajibu.
Taarifa za ndani kutoka Singida United zinasema pande zote mbili zimemalizana na kukubaliana kila kitu na sasa wanasubiri tu kumtambulisha rasmi Ajib kwa mashabiki wa Klabu hiyo yenye maskani yake mkoani Singida.
Hata hivyo Simba inaonekana kutoshtushwa na kuondoka kwa Ajib kwani ni kama tayari imejipanga kwa  kumalizana na John Bocco ambaye  takwimu zinaonesha ni mfungaji bora zaidi ya Ajib.
Kana kwamba haitoshi Singida United wapo mbioni kumchukua mlinda mlango wa Simba SC, Peter Manyika ili kujiimarisha na sfu ya ulinzi huku wakinyatia saini ya mshambuliaji wa Wekundu wa msimbazi ambaye hawakutaka kumuweka wazi kwa sasa.

Comments