Ikiwa leo ni siku ya kwanza kwa wanafunzi wa kidato cha sita kuanza mitihani yao ya Taifa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mhe. George Simbachawene ametoa onyo kwa wasimamizi wa mitihani hiyo.
Mh. Simbachawene amesema kuwa tabia ya wasimamizi kuwafanyia mitihani baadhi ya watahiniwa inatakiwa isiwepo kabisa wakati huu,na wanapaswa kuhakikisha wanazingatia kanuni na taratibu kwa kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote.
Aidha, Simbachawene amesema hakuna taarifa zozote za kuwapo kwa udanganyifu toka kwa wasimamizi na watahiniwa hao.
Jumla ya wanafunzi 75,155 wakiwamo wavulana 46,406 na wasichana 28,749, wameanza mitihani yao ya taifa katika vituo 577 vilivyopo nchi nzima.
Chanzo:ITV

Comments
Post a Comment