Mwanamuziki staa wa kike kutoka Bongoflevani Shilole maarufu kama ‘Shishi Baby’ amebainisha kuwa yupo mbioni kuvaa shela baada ya kupata mchumba ambaye tayari ameshakwenda kutambulishwa kwao.
Kupitia XXL ya Clouds FM Shilole amesema mchumba wake huyo ni mwenyeji wa Arusha na anatamani hiyo siku ya ndoa kila mtu ahudhurie: “Nimepata mchumba mwenyeji wa Arusha na tayari nimeshatambulishwa ukweni. Soon dada Mwajuma naenda kuvaa shela. Nataka ndoa yangu kila mtu ahudhurie, nijaze uwanja wa Taifa. Ndoa itafungwa juu ya ndege tutashukia uwanja wa Taifa.
Hata hivyo Shilole amesisitiza kuwa amekuwa akificha mahusiano yake akihofia kuyaweka wazi kwa sababu hata mahusiano yake ya awali yalivunjika kutokana na kuwekwa zaidi hadharani: “Mahusiano yangu ya nyuma yalivunjika kwa sababu niliyaweka wazi kwa watu wa karibu. Kwa sasa, namficha mume wangu mtarajiwa.” – Shilole.
Comments
Post a Comment