Sharapova anyimwa kadi maalum ya kuingia French Open

Sharapova hajaingia uwanjani kwa miezi 15 sasa
Sharapova hajaingia uwanjani kwa miezi 15 sasa
Nyota wa tenisi kutoka Urusi Maria Sharapova, amenyimwa kadi maalumu ya kuingia kwenye mashindano ya French Open yatakayoanza baadae mwezi huu.
Mkuu wa chama cha tenisi nchini Ufaransa Giudicelli Ferrandini mwaliko huo ungeliweza kutolewa kwa mchezaji ambaye ametoka kuwa majeruhi lakini sio kwa aliyefungiwa kwa kashfa ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli.
Sharapova, mshindi mara tano wa Grand Slam, alimaliza kifungo cha miezi 15 hivi karibuni na hakuwa na alama za kutosha za kuingia katika droo kubwa ya kushiriki michuano hiyo.

Comments