Setilaiti ndogo yaundwa na vijana wa shule

Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknologia, hatimaye setilaiti ndogo kuliko zote imetengenezwa nchini India.

Setilait aina ya KalamSat
Setilaiti hiyo iitwayo KalamSat, ikiwa ni jina la rais wa zamani wa India Abdul Kalam, ina uzito wa gram 64 na inatarajiwa kuwekwa kwenye mzingo wa dunia katika kituo cha shirika la safari za anga za juu la Marekani NASA mwezi Juni mwaka huu.
Setilaiti hiyo imetengenezwa na kijana kutokea nchini India aitwaye Rifath Shaarook mwenye umri wa miaka 18 akishirikiana na vijana wenzake watano ambao ni Vinay Bharadwaj, Tanishq Dwevdi, Yagnasai, Abdul Kashif na Gobi Nath ambao walishinda shindando lililoandaliwa na NASA pamoja na Kampuni ya elimu iitwayo idoodle.

Rifath Shaarook akipokea zawadi kwa niaba ya wenzake.
Shindano hilo lilipewa jina la ‘Cube in Space’,na liliweza kumuibua kijana huyo kutokea nchini India kuwa mshindi na kufanya setilaiti hiyo kuwa miongoni mwa setilaiti itakayotumika na itasafiri kwa kutumia muda wa dakika 12 katika mazingira sawa na ya angani.

Comments