Scott aringishia kimwana

Baada ya Scott Disick kutemana na mke wake miezi kadhaa iliyopita ameamua bora asonge mbele kwa kuamua kuopoa kimwana mpya wa kidachi aitwae Bella Thorne.

Scott Disick ameamua kuweka hali ya hewa sawa kwa upande wake kwa kumuhakikishia baby mama wake wazamani kwamba na yeye ameopoa kimwana mwingine.
Wawili hao wamenaswa wakijiachia siku ya jana katika jiji la Ufaransa maeneo ya Cannes Villa. Kitendo cha Scott kwenda mji huo kinamaasha kwamba amemfuata Kourtney ambaye yupo kwenye mji huo kumringishia amuone Bella.


Kourtney yupo kwenye mahusiano na Younes Bendjima, mahusiano ambayo yalianza kwa siri kwa muda na hatimaye mwezi huu mwanzoni walionekana pamoja kwa mara ya kwanza maeneo ya Beverly Hills, Magharibi mwa Hollywood wakiwa wanafanya shopping baada ya kumaliza kupata Lunch ya pamoja.

Comments