Sakata la mama aliyedai kuibiwa kichanga Temeke lachukua sura mpya

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa ameunda tume huru ya kuchunguza suala la mama ambaye amedai kuibiwa kichanga chake katika hospitali ya Rufaa ya Temeke.
Image result for ummy mwalimu
Waziri Ummy ameyazungumza hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo, jijini Dar es salaam huku akitoa siku 14 kwa tume hiyo kutoa majibu ya sakata hilo.
“Lakini niseme tu kwamba asubuhi nimekutana na Bi Asma Juma Elius ambaye ana madai ya kuibiwa kichanga chake katika hospitali ya Rufaa ya Temeke, kwahiyo nilielekeza mganga mkuu wa Dar es salaam afuatilie, wao wametuletea taarifa kuwa Bi Asma amekataa taarifa ya mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salaam. Kwahiyo baada ya kufuatilia hayo nikiwa Waziri mwenye dhamana lakini pia nikiwa na wajibu wa kutenda haki nimeamua kuunda tume huru ya kuchunguza suala hili, ambayo itaongozwa na Profesa Charles Majige daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama ambaye ndiye atakae kuwa Mwenyekiti pamoja na Bi Agness Mtawa ambaye ni muuguzi mkuu hospitali ya Taifa Muhimbili,” alisema Waziri Ummy.
“Lakini kwasababu kuna kubishania vipimo vya ultra sound, kwahiyo tuna mchukua mtaalam bingwa kutoka Muhimbili, yeye atatuambia kama ni watoto mapacha au sio mapacha lakini pia tuna daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama kutoka hospitali ya Mzena na mwakilishi mkuu wa serikali, kwahiyo nimewapa siku 14, baada ya siku 14 naamini watatuletea taarifa, na mwisho wa siku tunataka kutenda haki kama mama yule alikuwa na watoto mapacha au alikuwa na mtoto mmoja.”

Comments