Safari ya Simba kwenda FIFA imekwiva: Wadai hawaendi kusaka pointi tatu bali kudai haki

Klabu ya Simba kupitia kwa Makamu wa Rais wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ imetibitisha kupokea barua kutoka TFF ya kutupiliwa mbali kwa Rufaa yao dhidi ya Klabu ya Kagera Sugar ya kumchezesha Mohammed Fakhi ambaye alikuwa na Kadi tatu za njano, na kusema kuwa safari ya kwenda FIFA imekwiva.
Tokeo la picha la Kaburu simba
Makamu wa Rais wa Simba,Geofrey Nyange ‘Kaburu’
 
Kaburu amesema tayari wamepata barua kutoka TFF na huku akiweka wazi kuwa hawaendi huko kudai pointi 3 au ubingwa bali wanaenda kudai haki yao ambayo imekuwa ikiyumbishwa kila siku .
Ni kweli barua tumeipata na tuweke wazi tu kuwa nia ya kwenda FIFA sio kudai pointi 3 au kutaka Ubingwa hapana, nia ya kwenda FIFA ni kuona kwamba haki na matumizi sahihi ya kanuni kutoka kwenye vyombo vinavyosimamia mpira nchini ambavyo ndivyo vinasimamia kanuni na sheria vinafanya kazi kwa weledi “Alisema Kaburu jana kwenye uzinduzi wa Kampuni ya SportPesa.
Kuhusu tetesi za Klabu ya Simba kudhaminiwa na Kampuni ya SportPesa, Kaburu amesema taarifa zote zitatolewa Jumamosi hii.

Comments