Ni tunda linalopendwa sana na wengi lakini ndizi mara nyingi huwa hazitumiwi sana sana wakati wa kuandaa mchanganyiko wa matunda maarufu 'fruit salad', ambao unapangiwa kukaa kwa muda bila kuliwa.
Baada ya kutolewa maganda na kukatwakatwa, rangi yake hubadilika haraka kutoka manjano inayovutia na kuwa rangi ya kahawia, na mara nyingi huharibu matunda yale mengine yaliyochanganywa nayo.Lakini sasa huenda mambo yakabadilika.
Baada ya miaka mingi ya kujaribu, kampuni ya Marks and Spencer imebuni njia ya kuweka ndizi zikiwa safi na za kuvutia hata zinapochanganywa na matunda mengine.
Lakini kabla hatujajifunza ujuzi huu, ni vyema tuelewe kwa nini ndizi huharibika haraka.
"PPO hutokea wakati seli za mimea zinapoharibiwa kwa kukatwa," alisema.
"PPO hubadilisha kemikali za kawaida zinazoitwa 'phenolics' na kuzifanya ziwe 'quinones' na zinapochanganyika na oksijeni husababisha rangi ya kahawia."
Ni kwa nini basi ndizi huonekana kuharakisha kukomaa kwa matunda mengine pia?
"Ndizi hufanya matunda mengine kuiva kwa kuwa zinatoa gesi inayoitwa ethene (zamani ethilini)," aliongeza Dkt Bebber.
"Gesi hii husababisha kukomaa na kuiva kwa matunda na kuvunjika kwa kuta za seli, kupitia ubadilishaji wa wanga kuwa sukari na kupoteza asidi.
"Baadhi ya matunda, kama vile machungwa, hayaathiriki."
Kwa hivyo suluhisho ni nini?
Utafiti uliofanywa na M & S uligundua kuwa kwa kunyunyizia ndizi mchanganyiko wa tindikali au asidi ya citric na asidi ya amino, ndizi husalia kwenye hali nzuri na rangi yake ya manjano, bila kuathirika ladha.
Hii ni sawa na kutumia maji ya limau kuweka matunda safi.
Kampuni hii pia ilifanya utafiti ili kubaini ni aina gani ya ndizi ambazo huchukua muda mrefu kabla ya kuharibika na waligundua kuwa ndizi aina ya 'Cavendish' ndizo bora zaidi.
Comments
Post a Comment