RAY C ATOA DONGO WASANII WAKONGWE

Msanii mkongwe, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amewataka wasanii wenzake wakongwe kuamka na kuanza kushindana na wasanii wapya wa muziki ambao wanafanya vizuri kwenye game kwa sasa.

Muimbaji huyo, ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Unanimaliza’, amedai bado wasanii wakongwe wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika muziki.
“Wamekata tu tamaa ya maisha, lakini kuna wengi labda wanajua historia yangu tangu nilipotoka, nilipokuwa na mpaka sasa nimesimama hapa najua wanapata imani sana,” Ray C alikimbia kipindi cha Enewz cha EATV.
“Kwa hiyo nasimama hapa kama ‘hope’ kwa watu wengine ‘don’t give up’ kwenye ‘game’. Wasanii wengi wa zamani natamani niwasikie tena wakina Joslin, Juma Nature, Sister P, Raha P, Zay B, Daz Baba, Chid Benz, Daz Nunda, Feroouz pamoja na Fanani. Come back dada yenu nimepitia magumu labda kupita hata nyie lakini nipo hapa nimesimama ‘with a lot confidence’. Yaani sina hata muda wa kufikiria majuto, wasiwasi, uoga sijali kwamba watu watasemaje ndiyo maana mimi nimeweza, kwanini na wao wasiweze kwani wao ni wakina nani ?,” alisema Ray C.
Muimbaji huyo amesema wasanii wengi wanaogopa kurudi katika muziki kipindi hiki kwa kuhofia kutokuwa na mashabiki kama walivyokuwa zamani.

Jiunge na Hotmixmziray.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, ili kupata habari zote za town!

Comments