
Rais mpya wa Korea Kaskazini Moon Jae-in ameapishwa rasmi
Rais mpya wa Korea Kusini, Bwana Moon Jae-In, ameanza kazi rasmi afisini kwake baada ya kuapishwa.
Bwana Moon ametoa wito kupunguza uhasama kati ya Korea Kusini na Kaskazini na wakati huohuo kutaka kujua ni kwa nini Marekani iliweka makombora ya Ulinzi katika ardhi ya nchi yake.Amesema kuwa angependelea kutembelea Pyongyang katika hali nzuri.
Wakili huyo wa haki za kibinaadamu anayejulikana kwa maoni yake huria anataka kuimarisha uhusiano na Korea Kaskazini kinyume na sera iliopo kwa sasa.
Pia ameapa kuliunganisha taifa hilo linalokabiliwa na ufisadi ambao ulisababisha mtangulizi wake kushtakiwa mbali na kuimarisjha uchumi.
Mwanachama huyo wa chgama cha Democrat amejionyesha kuwa mtu ambaye anaweza kuliendesha mbele taifa hilo kutoka kwa ufisadi mbali na kuliunganisha.

Marekani na Korea Ksakazini zimekabiliana kimaneno katika majuma ya hivi karibuni baada ya Pyongyang kufanya majaribio ya makombora
Comments
Post a Comment