POSHO ZA WABUNGE LEO KWENDA KWA WAFIWA ARUSHA


 





Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo wakiwa bungeni wamekubaliana kwa kauli moja kuwa posho za kila mbunge kwa siku ya leo zipelekwe kwa wazazi wa wanafunzi waliofariki kwa ajali ya basi la Shule ya awali na Msingi ya Lucky Vincent.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaongoza waombolezaji mbalimbali kuaga miili 35 ya marehemu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Mbali na Makamu wa Rais pia viongozi mbalimbali wa Serikali wamewasili katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuaga miili ya wanafunzi waliofariki kwa ajali Arusha.

Comments