Abedi akiwa na sanduku lake la nguo
Polisi wa Uingereza wanaochunguza mlipuko wa Manchester wametoa taswira mpya kuhusu mshambuliaji, Salman Abedi, aliyebeba sanduku la nguo la rangi ya bluu.
Wanafanya uchunguzi ili kupata taarifa zake na kujua mizunguko yake ya siku nne nyuma kabla ya shambulizi, na wanaamini ni mmiliki wa sanduku la hilo la nguo.BBC pia imepata picha za CCTV zikimuonyesha Abedi akinunua chakula na kusafisha mazingira, siku moja kabla ya shambulizi.
Wanaume kumi na nne wako chini ya ulinzi wakihusishwa na shambulio hilo lililotokea wiki iliyopita.
Comments
Post a Comment