Picha: Mwalimu afukuzwa kwa kumburuza mwanafunzi wa miaka minne

Mwalimu mmoja huko Ohio Marekani amefukuzwa kwa kumburuza kijana mwenye asili ya kiafrika katika korido ya shule.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa WKBN amesema kuwa mwalimu Jenn Lohr amefukuzwa katika shule ya Alta Head Start kwa kumburuza kijana mwenye umri wa miaka minne mwenye asili ya watu weusi.
Mwalimu Jenn Lohr alikuwa akifundisha wanafunzi waliopo kwenye kundi la umri wa chini ya miaka 5 waliokuwa katika programu iitwayo Youngstown- Ohio ambao walikuwa jumla ya 854.P icha inayoonyesha mwalimu Lohr akimburuza mwanafunzi huyo ilipigwa na mwalimu mwingine mwenzake.
Mmiliki wa Alta Care Group, Joseph Shorokey amesema kuwa mwalimu huyo aliuambia uwongozi kuwa ilikua ni bahati mbaya, lakini uongozi ulisha ridhia kumfukuza kazi shuleni hapo.

Comments