Katika ulimwengu wa soka jina la staa wa Man United Paul Pogba sio jina geni masikioni mwa mashabiki wa soka ambapo ndio Mchezaji aliyesajiliwa kwa dau kubwa duniani kuliko mchezaji yoyote, leo February 6 2017 zimetoka picha za mjengo mpya alioununua ukiwa umbali wa dakika 20 kutoka uwanja wa mazoezi wa Man United ulipo.
Nyumba hiyo ya Pogba iliyopo Cheshire imemgharimu pound milioni 2.9 ambazo ni zaidi ya Bilioni 8 za kitanzania na unaambiwa hiyo ni baada ya punguzo la pound 600,000 kutoka bei ya awali ya nyumba hiyo yenye vyumba vitano vya kulala, sehemu ya games na nakshinakshi mbalimbali ikiwemo swimming pool.
Comments
Post a Comment