PFUNK AMPONGEZA DARASA


Katika kutambulisha kundi jipya kutoka Bongo Records, producer mkongwe wa Bongo Fleva P Funk Majani ameongelea ushawishi mkubwa kutoka kwenye uimbaji wa Darassa.
P Funk anasema mtindo wa Bounce wa Darassa umemshawishi kufanya aina flani ya muziki na kuupeleka mbali zaidi mtindo huo…

P Funk anasema Nampa respect nyingi sana Darassa yeye ni namna moja au nyingine mimi kuja na hili ‘bounce’ ni ushawishi kutoka kwa Darassa hivyo nimeipeleka sehemu nyingine, kuna watu walikuwa wanang’ang’ania sana oohh Darassa, Darassa tunataka kitu fulani kama Darassa kwa kuwa mimi huwa siwezi ku copy nikakwepa hilo na mzigo nitatengeneza ndiyo huo. Napenda style ya Darassa kwa kuwa ni simple unamsikia neno kwa neno na kuwa na simple siku zote inauza

Comments