Paka huyu wa aina ya Maine Coon ana urefu wa sentimita 120
Omar alikuwa na ukubwa sawa na paka wengine wote waliokuwa wakiishi pamoja naye, kabla yake kuchukuliwa na mmiliki wake Stephy Hirst, mwaka wa 2013.
Lakini sasa paka huyu wa aina ya Maine Coon kutoka Melbourne, Australia ana urefu wa sentimita 120 (futi 3, inchi 11) na huenda akawa ndiye paka mrefu zaidi duniani aliyefugwa.Baada ya sifa zake kuenea mitandaoni, Hirst anasema Guinness World Records waliwasiliana naye na kumuuliza kipimo cha paka wake.
Anayeshikilia rekodi kwa sasa ni paka aina ya Maine Coon kutoka Wakefield, West Yorkshire aliye na urefu wa sentimita 118 (futi 3, inchi 10.59).
Hirst alianza kuchapisha picha zake Omar kwenye mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita na moja kati ya picha hizo ilisambazwa zaidi ya mara elfu 270 katika mtandao wa kijamii wa Instagram.
"Bado hajazoea umaarufu huu wote," Bi Hirst aliiambia BBC.
"Alikuwa ametatizika kidogo leo asubuhi."
Kwa kawaida Omar huamka saa kumi na moja asubuhi.
Yeye hula chakula chake na kisha kucheza nyumbani au uwanjani, kabla ya kupumzika. Chakula chake cha jioni huwa ni nyama ya kangaroo.
"Sisi hununua nyama ya kangaroo kwenye maduka makubwa makubwa, ni nyama sawa na ile inaliwa na binadamu," Bi Hirst alisema. "Hiyo tu ndio nyama anayoweza kula."
Mnyama huyo huwacha manyoya yake kila mahali anapopita ndani ya nyumba. Ana uzito wa kilogramu 14 na ni vigumu kumuinua kila mara.
Omar pia ana talanta ya kufungua milango na kabati za nguo na vyombo.
"Marafiki zetu wote hutaka kuja kumuona Omar," Bi Hirst alisema.
Baada ya Guinness World Records kudhibitisha ukubwa na urefu wake, inaweza kuchukua jumla ya wiki 12 kutoa majibu.
Comments
Post a Comment