Melania Trump alifuata kanuni akikutana na Papa akiwa na Donald
Melania Trump aliwasili Vatican akiwa amevalia nadhifu, nguo ndefu, mikono imefunikwa na kujifunika kitambaa cheusi kichwani.
chaguo lake la mavazi hususan kitambaa cheusi, kilitambuliwa sana na wale wanaomfuatilia kwa karibu mama huyo kwa kwanza wakati wa ziara ya kwanza ya mumewe nchi za kigeni.Kwa kawaida kuna kanuni kali zinazostahili kufuatwa wakati wa kukutana na Papa ambazo White House ilijulishwa.
Kitamaduni viongozi wa nchi na wake zao huchagua kuvaa nguo nyeusi.
Watangulizi wake Trump wamefuata kanuni hizo kali. Michelle Obama alichagua kuvaa kitambaa kichwani wakati alimtembelea Papa Benedict mwaka 2009 kama walivyofanya Laura Bush na Hillary Clinton.
Hata hivyo kuna wengine ambao wanapuuza kanuni hizo.
Kwa mfano kulitokea malalamiko wakati Cherie Bliar, mke wa aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza alivaa nguo nyeupe mwaka 2006, na pia wakati Camilla, mke wa Prince Charles alivaa suti nyeupe bila hata kujifunika kichwa.
Comments
Post a Comment