Nandy amtaja mshindani wake katika Bongo Fleva

Msanii Nandy amesema changamoto kubwa katika muziki wake kwa sasa ni kuhakikisha anaendelea kuwa juu huku akimtaja Maua Sama kuwa ni miongoni mwa msanii ambao anawachukulia kama washindani wake wakubwa katika muziki.
Nandy
Nandy ameimbia TBC Taifa kuwa changamoto anayoipata kwa sasa ni ushindani kutoka kwa wasanii wenzake wa kike.
“Yaani nikija kutoa wimbo usishuke au uwe juu zaidi, au nifanye ubunifu gani kutofautiana na wenzangu ili niweze kubakia katika nafasi yangu. Wasichana wote kwenye industry wapo katika ushindani  kwa sababu tunafanya biashara moja, kwa hiyo ninapomuangalia mtu kama Maua namuangalia kwa jicho la kama msanii mwenzangu, kwa jicho la kibiashara, kwa hiyo namuangalia kama mshindani wangu,” ameeleza Nandy.

Comments